top of page

AZAM 0 - YANGA 2: Hall atumia mfumo wa 4-4-2

Ally Mustafah
Oscar Joshua
Mbuyu Twite
Nadir Haroub
Kevin Yondan
Athumani Iddi
Frank Domayo
Haruna Niyonzima

Didier Kavubamgu

Hamisi Kiza

Simon Msuva

Ally Mwadini
Ibrahim Shikanda

Ereasto Nyoni
Said Mourad
Aggrey Morris

Kipre Balou
Salum Abubakar

Khamis Mcha
John Bocco
Jabir Aziz
Kipre Herman Tchetche

Yanga: 4-4-2

Azam: 4-4-2

Mchezo wa leo haukuwa mzuri kama vile ulivyotegemewa kutokana na Azam kutocheza vizuri. Hii ni mara ya pili Azam anafungwa ndani ya wiki moja, akipoteza michezo yote dhidi ya Simba na Yanga, timu ambazo ndio wapinzani wake wakuu katika kuwania ubingwa. Hall ana kazi ya ziada kama Azam watatwaa ubingwa mwisho wa msimu.
 

Yanga walitumia mfumo wao wa 4-4-2 huku Chuji akicheza chini kidogo ya Domayo. Tatizo kuu kwa upande wa Azam kipindi cha kwanza ilikuwa kushindwa kumiliki mpira kwenye nusu ya wapinzani wao, huku mipira mingi ikinaswa na mabeki wa Yanga. Walijaribu penyeza mipira nyumba ya mabeki wa Yanga kumtafuta Boko lakini mara kadhaa alijikuta akiwa katika nafasi ya kuotea.
 

Mbinu kuu ambayo Azam utumia katika mashambulizi ni kwa Kipre Tchetche au Boko kukimbilia kwenye nafasi kati ya beki wa pembeni na beki wa katikati hasa pale ambapo beki wa pembeni amependa kushabulia. Mara kadhaa walikimbilia upande wa kulia wa Yanga ambapo Twite alikuwa akicheza. Hii nikutokana na kwamba Twite anapanda sana ilikujiunga na mashabulizi. Yanga walijihakikishia ulinzi kwa kuacha mabeki watatu nyuma wakati wanashambulia. Beki wa kushoto, Joshua alibaki nyuma wakati Twite alipojiunga na mashambulizi.
 

Kipindi cha pili Azam walionekana kucheza vizuri ukilinganisha na kipindi cha kwanza. Baada ya kutambua kuwa mipira mrefu nyuma ya mabeki wa Yanga ilikuwa haina madhara yoyote na Boko kujikuta akiwiwa kwenye nafasi za kuotea, Boko alianza kupokea mipira mguuni baadala ya kwenye njia. Hii iliwawezesha Azam kuweza kumiliki mpira kwenye nusu ya wapinzani wao lakini hawakutengeneza nafasi za wazi. Goli la pili lilipatikana baada ya Morad na Nuhu kuchanganyana. Morad alijikuta yupo katika upande wa kushoto na Nuhu akilinda nafasi yake katikati. Katika jitihada za kujaribu kurudi katika nafasi zao, Chuji alipokea mpira na kujikuta katika nafasi ya kupiga krosi ambaye Kiiza aliweza kukutana nayo na kufunga. Baada ya hapo, wachezaji wa Azam walionekana kuvinjika moyo.
 

Tatizo kubwa la Azam chini ya uongozi wa Bunjak ulikuwa uwembamba wa mfumo aliokuwa anautumia. Uamuzi wa Hall kutumia 4-4-2 unaonekana ulilenga kutatua tatizo hilo hasa wakati wa kukaba. Upana unaoletwa na mawinga wa 4-4-2 ungeleta ulinzi zaidi kwenye maeneo ya pembeni na hivyo ungeweza kuzuia mipira ya krosi ambayo ndio yaliwatatiza katika mechi dhidi ya Simba.
 

Uamuzi wa kumchezesha Salum Abubakar kama winga wa upande wa kulia ulikuwa wa mashaka ukizingatia kuwa yeye ni kiungo wa kati. Mechi dhidi ya Simba alicheza kama kiungo mshambuliaji nyuma ya Boko na Kipre Tchetche. Kuna kipindi alikuwa anajisahau na kushuka chini maeneo ya kati kupokea mpira kama vile anacheza kama kiungo wa kati. Goli la kwanza la Yanga lilitoka upande huu baada ya Erasto Nyoni kushindwa kuutoa kwenye eneo la hatari.
 

Hall alijaribu kurekebissha matatizo ya udhaifu wa kukabiliana na mipira ya krosi. Ukizingatia kuwa alikuwa na siku kadhaa tuu za kufanya kazi na wachezaji, itakuwa vigumu sana kumulaumu kwa kufungwa mechi hii. Jitiada za ziada zitaitajika kurekebisha mapungufu yao. Pia itabidi atafute mbinu mbadala za kushambulia kutokana na mbinu ya sasa kuwa inatabirika na wapinzani wameshapata mbinu za kukabiliana nayo.

bottom of page