top of page

IShaaban Hassan Kado
Malika Ndeule
Issa R Issa
Dickson Daudi
Salvatory Ntebe
Shaaban Nditi
Jamal Mnyate
Awadh Juma

Hussein Javu

Shaaban Kisiga

Vincent Barnabas

Ally Mustafa
Juma Abdul
Mbuyu Twite
Nadir Haroub
Kevin Yondan
Athumani Iddi
Frank Domayo
Haruna Niyonzima

Said Bahanuzi

Hamisi Kiza

David Luhende

Yanga wamepokea kipigo cha magoli tatu bila majibu katika uwanja wa Jamhuri Morogoro. Mtibwa walijipanga katika mfumo wa 4-2-3-1 huku Yanga wakitumia ule wa 3-4-1-2. Niyonzima alicheza nyuma ya Kiza na Bahamuzi. Jambo la kushangaza ni kwamba kabla ya mchezo kuanza chuji alisimama katika nafasi ya beki wa pembeni wa kushoto na hivyo mfumo wa Yanaga kuonekana kama 4-4-2. Hii ilikuwa mbinu ya kujaribu kuwachanganya wapinzani juu ya mfumo ambao wangetumia. Mchezo ulianza vizuri huku timu zote mbili zikijaribu kuanzisha mashambulizi toka nyuma na kutumia pasi fupi fupi.

Ilikuwa dhahiri kuwa mbinu ya Mtibwa ni mpira kupita kwa Nditi ambaye ange sambaza pasi kueleka washambuliaje wa pembeni. Mtibwa walifanikiwa kutengeneza nafasi ndani ya dakika sita za mwanzo kwa kutumia mbinu hii. Nditi alicheza mbele ya mabeki wake wanne ila alielemea upande wa kushoto.

Goli la kwanza la Mtibwa lilipatikana kupita kona iliyo pigwa kwenye upande wao wa kushoto. Mashambulizi mengi yalielekezwa upande huu wa uwanja na inaonekana ndio upande wenye washambuliaje wazuri maana ata walipo cheza dhidi ya Polisi Moro walitumia upande huu wa kushoto.Mshambuliaje wa pembeni na fullback wake walihusika katika kushambulia  huku Nditi akijiunga pia na kutengeneza hali ya 3 dhidi ya 3 katika upande huu wa uwanja. Kuelemea kwa mchezo upande huu wa uwanja ulimaanisha kuwa upande wa kulia ulikuwa wazi na mara kadhaa Nditi alijaribu piga mpira mrefu kuelekea upande huo lakini pasi zake hazikuwa nzuri.

Walipokuwa wanalinda goli lao Mtibwa walijipanga 4-4-2 lakini nditi alikuwa chini zaidi hivyo kuufanya mfumo uonekane kama 4-1-3-2. Kiza na Bahamuzi hawakuhusika katika ukabaji pale Yanga walipopoteza mpira. Fullback wa kulia wa Mtibwa aliingia ndani na kucheza karibu na mabeki wake wa kati pale ambapo walikuwa wanashabulia upande wa kushoto. Hii ili hakikisha kuwa kila wakati wao watatu wanacheza dhidi ya washambuliaji wawili ya Yanga.

 

Udhaifu wa Yanga.​

Yanga walionekana wenye kupoteza mwelekeo baada ya Mtibwa kupata goli la kwanza. Waliacha kucheza pasi fupi fupi na baadala yake kupiga pasi ndefu. Walianza poteza mipira huku Mtibwa wakishinda mipira mingi ya hewani kupitia wachezaji wao warefu Nditi na Daudi. Tatizo halikuishia hapo tuu bali hata mipira ya kugombania wachezaji wa Mtibwa ndio walikuwa wakwanza kuipata na kukaa nayo na kumtumia Nditi kuwawezesha kumiliki mpira.

3-4-1-2 ni mfumo ambao unatumia wingbacks. Hawa wana jukumu la kucheza kama winga na kama beki wa pembeni. Pia wao ndio uipa timu upana wakati wa kushambulia. Wingback wa kulia wa Yanga aliweza kupokea mipira ila tatizo lake kuu ilikuwa kushindwa kuitumia vyema huku akiishia kutoa basi au krosi mbovu na kuisha kupoteza mpira. Yanaga wakaanza kushambulia upande wa kushoto kwao baada ya kuona kuwa wanapoteza sana mipira upande wa kilia. Walifanikiwa upande huu kupata kona kadhaa ila kona zao hazikuwa zenye madhara kwenye lango la wapinza wao. Nafasi ya wazi waliipata kupitia mpira wa adhabu ambao mlinda mlango Kado aliutema lakini Yanga walishindwa kuumalizia.

Kwa kucheza na mabeki watatu Yanga walijipunguzia idadi ya wachezaji wanaohusika kati mashambulizi. Hili ndio tatizo kubwa pale ambapo mabeki watatu wanacheza dhidi ya mshabuliaji mmoja. Yondani alicheza kama sweeper huku Nadir Haroub na Twite walicheza kama wakabaji. kwa kuwa walikuwa wanacheza dhidi ya mshambuliaji mmoja basi kulikuwa hamna haja ya kucheza na wakabaji wawili. suluhisho rahishi ni kwa hawa wawili kuhusika katika mashambulizi zaidi  kwa kupanda na mpira mpaka maeneo ya katikati ya uwanja. Njia nyingine ni kumsogeza Yondani acheze mbele ya hao wakabaji wawili. kwa kufanya hivyo inegemsogeza Chuji juu zaidi na hivyo idadi ya wanaohusika katika kushambulia kuongezeka. (kama utatumia mbinu ya pili basi ni bora kabisa ukaondokana na huyo sweeper na kubakia na mabeki wawili dhidi ya mshambuliaji mmoja)

 

Uzembe wa mabeki kuruhusu mpira kudunda ndio ulio sababisha goli la pili. Ukizingatia kuwa mfumo waliokuwa wanatumia ulitokana na kujaribu kukabiliana na tukio kama hili ni dhahiri kuwa Satintfiet atakuwa amesikitishwa sana na jambo hilo.

Kipindi cha pili

Yanga walibadilisha mfumo baada ya kuonekana kuwa wachezaji hawakuelewa majukumu yao katika mfumo wa 3-4-1-2.  Twite alicheza katiti na Chuji katika mfumo wa 4-2-3-1. Mabadiliko hayo yalionyesha kuleta utuvilivu huku Yanga wakiwa wameongeza kasi ya mashambulizi. Mtibwa waliendelea kupitisha mashambulizi yao upande wao wa kushoto huku mshambuliaji wao wa pembeni akioneka kuwa mwenye mbio kuliko mabeki wa Yanga. Yanga nao walishambulia kupitia upande wao wa kushoto ambapo Mwasyika alikuwa anacheza kama beki namba tatu. Nafasi mbili walizoweza tengeneza kipindi cha pili zilitokea upande huu wakushoto.

 

Kwa ufupi wachezaji wa Yanga walionyesha kutoelewa majukumu yao katika mfumo wa 3-4-1-2. Kutokana na kucheza vibaya leo kwa kutumia mfumo huu haitakuwa ajabu kuona Saintfiet akitumia mfumo wa 4-2-3-1 dhidi ya JKT Ruvu jumamosi.

Mabeki watatu dhidi ya mshambuliaji mmoja. hii iliwapunguzia Yanga idadi ya wachezaji walihusika kwatika mashambilizi.

Mtibwa: 4-2-3-1

Yanga: 3-4-1-2

MTIBWA 3 – YANGA 0:  Mfumo wa 3-4-1-2 wachangaya wachezaji

bottom of page