top of page

Juma Kaseja
Nassor Masoud
Amir Maftah
Paschal Ochieng
Shomary Kapombe
Mkude
Mrisho Ngassa

Mwinyi Kazimoto
Felix Sunzu
Amri Kiemba
Emanuel Okwi

Simba: 4-2-3-1

Polisi Moro: 4-1-3-2

Simba wameendeleza wimbi la sare mechi za ugenini baada ya kulazimishwa sare na Polisi Moro katika uwanja wa Jamhuri. Wachezaji walioanza kwa upande wa Simba ni kama ilivyotegemewa wakitumia mfumo wao wa 4-2-3-1 huku Mkude akiwa kama kiungo mkabaji na Kiemba akicheza mbele kidogo.
Kumekuwa na malalamiko mengi kuhusu hali ya kiwanja cha Jamhuri na wengi kutumia hiyo kama sababu yakutocheza mchezo mzuri. Simba waliweza cheza mchezo wao wa pasi fupi fupi na hivyo kudhihirisha kuwa hayo ni madai yasiyokuwa na ukweli.

 

Kipindi cha kwanza:
Polisi walianza mchezo kwa kasi na waliweza tengeneza nafasi mbili za kwanza za mchezo. Y a kwanza ilikuwa kupitia Kona nay a pili krosi, zote zikitokea upande wwao wa kulia. Baada ya hamsha hamsha hizi, Simba waliweza kutawala mchezo kwa kucheza pasi fupi fupi . Katikati ya uwanja walikuwa wanacheza viungo watatu wa samba dhidi ya wawili wa Polisi. Mkude alijikuta akiwa huru na hivyo alihakikisha kuwa Simba wanamiliki mpira kwa kusambaza pasi pembeni .
Mbinu ya Simba ilikuwa kujaribu kupenyeza mpira nyuma na mabeki wa Polisi. Walijaribu hivyo kupitia upande wa kulia ambako Ngassa alikuwa ameanza, wakijaribu kutmia kasi yake. Pia Kaseja alijaribu kupinga mpira mirefu ili Okwi na Ngassa waikimbilie. Pamoja na kujaribu kufanya hivyo pia walijaribu pasi za gonga kwenye maeneo nje ya aneo la penati ila hawakufanikiwa  kwa kuwa pasi zilikuwa ndefu au kukosea katika utoaji wa pasi.

 

Okwi:
 

Kwa ujumla Okwi hakuwa na mchezo mzuri. Alianza mcehzo wa leo akiwa upande wa kushoto na kwa kipindi hicho, Polisi ndio waliweza tengeneza nafasi zao mbili za mapema kupitia upande huu. Baadae alibadilishana upande na Ngassa na ghafla mashambulizi mengi ya polisi yalihamia upande ambao Okwi alikuwepo.  Hii ni kwa sababu Okwi hahusiki sana katika ukabaji na hivyo beki wa kushoto wa Polisi aliweza kupanda bila pingamizi. Hii ilitengeneza hali ya 2 v 1 dhidi ya Masoud na Polisi walifakiwa pata kona kadha. Akabadilisha tena upande na kurudi upande wa kushoto wa Simba. Huku alipokea mpira na kuupoteza na sekunde chache baadae Polisi walipata goli lao, shambulizi likiwa limeanza baada ya Okwi kupokonywa mpira. Ni jambo la kawaida la mchezaji mahiri kutohusika katika ukabaji  ila inabidi kuwe na mbinu za kuficha udhaifu wake, jambo ambalo leo Simba hawakuweza kufanya.

Mkude:
 

Mkude ndio alikuwa nyota wa mchezo. Uwezo wake wakujiweka kwenye nafasi sahii kwa wakati sahii ndio uliwawezasha Simba kutawala dimba. Aliweza sambaza pasi kuelekea pembeni na pia kucheza pasi za gonga na Kiemba. Kwa uwezo alioonyesha leo ni wazi kwa nini Kazimoto amesogezwa mbele acheze nyuma ya Sunzu na Mkude kucheza kama kiungo Mkabaji. Kazimoto ni mzuri katika kushambulia hasa mashuti ya mbali na hivyo kutakuwa na manufaa zaidi kwa yeye kucheza kama kiungo mshambuliaji. Kipindi cha pili, Mkude alianza piga pasi ndefu. Alipoteza kadhaa lakini ukizinga kuwa Simba kwa wakati huo walikuwa wanatafuta goli la ushindi, hivyo basi alikuwa anajasiri pasi zake.

Kipindi cha pili:
 

Kipindi cha pili Simba walianza mchezo kwa kasi. Mashambulizi yao yalipitia upande wa kulia. Mabadiliko ya kipindi cha pili hayakuubadilisha sana mchezo kiufundi. Akuffo aliingia nafasi ya Ngassa. Sunzu alienda kucheza kama mshabulia wa pembeni kulia, Okwi kushoto na Akuffo katika. Goli la Simba lilipatikana baana ya mabeki wa Polisi kushindwa kucheza mpira wa pili baada ya kona. Kona hii ilipatikana baada ya  kona fupi kuokolewa iloyopatikana upande wa kulia ambako mashambulizi ya Simba yalipitia.
 

Nafasi ya Polisi kipindi cha pili ilipatikana kupita mpira wa kona. Wakati wa kulinda dhidi ya kona ya washambuliaji, mwamba wa kwanza ulindwa na Sunzu. Wakati kona inapigwa Sunzu alibakia katikati ya uwanja  na hivyo hili eneo lilikuwa halina uliza na mchezaji wa Polisi alifanikiwa kukutana na mpira huo wa kona ila mpira ulipita pembeni.

Hitimisho:
 

Mchezo ulikuwa wenye kusisimua na Simba aliutawala kwa kipindi kirefu. Udhaifu wa Okwi wakati wa ukabaji na safu ya ushambuliaji kushindwa tengeneza nafasi nyingi za wazi ndio kilicho waangusha Simba.

POLISI MORO 1 - SIMBA 1: Udhaifu wa Okwi waonekana

Samahani, orodha ya wachezaji hakupatikana.

bottom of page