top of page

Juma Kaseja
Nassor Masoud
Amir Maftah
Juma Nyoso
Shomary Kapombe
Ramadhan Chombo
Mrisho Ngassa

Mwinyi Kazimoto
Daniel Akuffo
Amri Kiemba
Felix Sunzu

Benjamin Haule
Michael Pius
Mau Bofu
George Michael
Said Suzan
Gideon David
Abdulrahman Mussa
Hassan Dilunga
Paul Ndauka
Hussein Said
Said Dilunga

Simba: 4-2-3-1

R. Shooting 4-1-3-2

Simba amefanikiwa kushinda mechi yake ya tatu mfululizo katika ligi. Ilikuwa mechi ya vipindi viwili ambapo Simba alifanikiwa kutawala mchezo kwenye kipidi cha kwanza  na kulegalega kipindi cha pili.



Kipindi cha kwanza



Simba walikuwa wakitumia mfumo wa 4-2-3-1 huku Shooting ule wa 4-1-3-2. Simba aliweza kutawala mchezo kipindi cha kwanza kwa sababu alikuwa na mchezaji mmoja wa ziada katikati ya uwanja. Mfumo wa 4-1-3-2  unakuwa na viungo wawili katika huku ule wa 4-2-3-1 ukiwa na viungo watatu. Kiungo wa ziada alikuwa Chombo ambaye alifanikiwa kupokea mipira katikati ya mistari ya mabeki na viungo wa Shooting. Baada ya kuona kuwa Chomboanapata mwanya wakupokea mipira, kiungo mkabaji wa Shooting aliamua kumganda Chombo. Hii ilipunguza idadi za pasi ambayo Chombo alipokea lakini Kazimoto na Kiemba walikuwa wanacheza dhidi ya kiungo mmoja wa Shooting ambaye alishindwa kukabiliana na hawa watu wawili. Matokeo yake ni kwamba Kazimoto alijikuta yupo huru na alifanikiwa kupinga mashuti mawili kuelekea lango la wapinza. Goli la Simba lilipatikana baada ya Kazimoto kupanda na mpira na kumpasia beki wake wa kulia Masoud. Sunzu alimalizia krosi nzuri ya Masoud na kuwapa Simba goli lao la kwanza.

Viungo watatu wa Simba dhidi ya wawili wa Shooting. Hali hii iliwawezesha Simba kutawala mchezo katika kipindi cha kwanza.

Pamoja na kutawala mchezo kwa muda mwingi Simba hawakufanikiwa penyenza mipira nyuma ya mabeki wa Shooting. Ngasa alicheza upande wa kushoto na alipo pokea mpira alikimbia kuelekea katikati ya uwanja.  Tatizo ilikuwa kwamba Chapombe hakupanda sana ili kuwatanua mabeki wa Shooting na pia kutumia nafasi alitoacha Ngasa kwa kukimbilia ndani. 



Mashambulizi mengi ya Shooting yalipitia upande wao wa kulia. Waliweza kukwepa ukabaji wa Simba ila tatizo mashambulizi yao mara nyingi yalikwama pale walipo ingia kwenye nusu ya wapinzani.  Nafasi yao ya wazi katika kipindi cha kwanza ilipatikana kutoka upande huu baada ya krosi  kukutwa na kichwa cha mshambuliaji ambaye aliupaiza mpira juu ya mwamba.



Jambo lengini ni kwamaba wakati Simba walikuwa wanalinda goli lao wakati wa mpira wa kona, Sunzu alilinda eneo lililo karibu na mwamba wa mbele. Kona ya kwanza ya Shooting yeye aliweza kuiokoa. Kona zingine za Shooting zilikuwa zikilenga kumkwepa Sunzu. Ya pili walicheza kona fupi na ya tatu walijaribu kupeleka mpira mwamba wa mwisho ila mpira ilitoka kabla ya kurudi tena ndani.

Kiemba alikuwa anapoteza pasi and kuporwa na Shooting mara mbili waliweza kuanzisha mashabulizi  ila kama mashambulizi yao mengi yaliishia kutokuzaa matunda.



Kipindi cha pili



Katika kipindi cha pili mifumo ilibakia vilevile  ila Kazimoto alikuwa akicheza upande wa kushoto ambapo mwanzoni alikuwa anacheza upande wa kulia pale katikati. Simba hawakuwa wanatawala dimba kama kipindi cha kwanza na mchango wa Chombo katika midfield ulififia na hatimaye kufanyiwa mabadiliko.

Mashambulizi ya Shooting yalikuwa sasa yanapitia upande wa kushuto. Mara kadha walifanikiwa kupitisha mpira maeneo ya kati. Hii ilitokana na kwamba Ngasa alikuwa anacheza juu kidogo ya Kazimoto na Kiemba  wakati wa ukabaji.



Shooting walizawadiwa goli baada ya Kaseja na Nyoso kulazimisha kuanzisha mashambulizi toka nyuma. Baada ya hapo Shooting walionekana kuridhika na sare. Walianza kupoteza mipira kwa kupiga mipira mirefu na mmoja wapo ulichukuliwa na mabeki wa Simba ambao walianzisha mashambulizi kupita Ngasa ambaye sasa alikuwa akicheza upande wa kulia. Pasi yake kwa Edward ilizaa goli la ushindi.



Simba waliweza kutumia vizuri faida ya kuwa na mtu mmoja wa ziada pale katikati hivyo kujenga hali ya 3 v 2 katika kipindi cha kwanza. Tatizo ni kwamba walishindwa kutawala kipindi cha pili ijapokuwa mifumo ilibakia vilevile.

SIMBA 2 – R. SHOOTING 1:  4-2-3-1 VS 4-1-3-2 

bottom of page