TREQUARTISTA
FORMATIONS, STRATEGIES AND TACTICS
SIMBA 3 – AZAM 2: Simba watumia udhaifu wa 4-3-1-2

Simba: 4-2-3-1

Azam: 4-3-1-2
Mechi ya ngao ya hisani ilikuwa yenye kuburudisha na iliyojaa mbinu. Azam walianza mechi kwa kasi na kufanikiwa kupata goli namo dakika ya pili ya mchezo kupitia kona nzuri waliocheza. Dakika za mwanzo wachezaji wa Simba walioneka wakiwa bado hawaja changamka. Hii ilitokana na warm-up yao kutokuwa nzuri na kuchukua dakika tisa pungufu ukilinganisha na ile ya Azam.
Simba walitumia mfumo wa 4-2-3-1 huku Azam wakitumia ule wa 4-3-1-2. Mfumo wa Simba una upana kwa kuwa na washambuliaji wawili pembeni mmoja kila upande huku ule wa Azam ukilenga kutawala dimba kwa kuwa na watu wanne dhidi ya watu wa 4-2-3-1. Mbinu za azam ilikuwa kujaribu kucheza kwa counter-attack huku washambuliaji wake wawili Boko na Tchetche wakikimbilia pembeni na kuanzisha mashambulizi. Mbinu hii ndio uliwapa Azam upana ukizingatia kuwa mfumo waliokuwa wanatumia hauna wachezaji wa pembeni. Mashambulizi mengi ya Azam yalitokana na Simba kupoteza mpira ndani ya nusu ya maadui na kutegemea kupata faulo. Huku mabeki wa pembeni wa Simba wakiwa wamepanda, Boko/Tchetche walikimbilia kwenye nafasi ambayo hawa mabeki wameiacha wazi. Nyendo za hawa washabuliaji wawili zilikuwa zenye hatari na zilizaa matunda kwa kuwapatia Azam goli lao la pili.
Walipo poteza mpira Azam walizingatia kupanga mistari yao na kulinda eneo la katikati. Hawakujaribu kuufuata mpira kwenye nusu ya wapinzani na hii ilimmanisha kuwa mchezaji wao wa ziada katika hili eneo alipotea kwa kuwa alikuwa akicheza mbele ya viungo wawili wa Simba Kazimoto na Haruna moshi. Alipo jaribu kuwapora mpira ilishindikana kutokana na kujikuta akikabiliana na wachezaji wawili.
Wembamba wa mfumo wa 4-3-1-2 uliwawezesha simba kutumia upana wa uwanja ambapo kulikuwa na nafasi na hivyo kutawala mchezo
Kadri kipindi cha kwanza kilivyoendelea Simba walianza kutumia udhaifu wa mfumo wa 4-3-1-2 ambao ni uwembamba wake. Mashambulizi yao yalipitia sana upande wao wa kulia. Tatizo kubwa ni kwamba pasi nyingi zilikuwa kuelekea mguuni na sio kwenye njia au nyuma ya mabeki wa Azam. Lengini ni kwamba pale walipofanikiwa kupenya pasi za mwisho zao hazikuwa na madhara katika lango la Azam. Simba walifanikiwa kupata penati baada ya beki wa Azam kushika mpira kwa mkono. Okwi na Ngasa walikuwa wakibadilisha upande mara kwa mara. Tofauti kati yao ilikuwa kwamba Okwi alikuwa anapenda kuuingia ndani na kupokea mpira kwenye nafasi iliyo katikati ya mabeki na viungo wa Azam wakati Ngasa alikuwa akikaa pembezoni mwa uwanja. Mwenendo wa Okwi uliwapatia simba mipira ya adhabu kadhaa ila iliwanyima upana upande wa kushoto.
Kipindi cha pili Simba walikuja wakicheza kwa mapana na Okwi hakuoneka akiikimbilia maeneo ya katikati tena. Simba ikiwa inatawala mchezo Azam walijikuta wakiwa wamebanwa kwenye nusu yao huku Kazimoto akipata muda na nafasi ya kusambaza pasi pembeni. Alitumia uhuru huu kuipatia Simba goli la tatu kwa shuti nje ya eneo. Azam waliendelea na mbinu yao ile ile na kufanikiwa kutengeneza nafasi za wazi moja yapo baada ya Boko kufanikiwa kupenyeza mpira kwa Tchetche ambaye baada ya kumzunguka Kaseja hakufanikiwa kulenga goli. Muda ulivyoenda washanbuliaji hawa wawili walianza kuonyesha dalili za kuchoka na labda mabadiliko ya Tchetche yangefanywa mapema zaidi.
Magoli mawili ya Simba katika kipindi cha pili yalitokana na ufundi binafsi wa Okwi na Kazimoto ila pongezi ziende kwao kwa kucheza kwa upana hivyo kutumia udhaifu wa mfumo wa 4-3-1-2. Hata hivyo Simba hawakutengeneza nafasi za wazi ukilinganisha na Azam. Lawama lazima iende kwa kocha wa Azam Bunjak, kwa kushindwa kukabiliana na udhaifu wa mfumo aliotumia. Kama Azam watendelea kutumia mfumo huu basi nilazima warekebishe mambo kadhaa
1) Hakikisha wanatawala dimba kwa kuwa mfumo wao unaidadi kubwa ya watu maeno ya katikati
2) Majukumu ya kiungo mchezeshaji yajulikane
3) Mabeki wa kati wawe na uwezo wa kuanzisha mashambulizi toka nyuma na sio kupiga pasi ndefu zinazo ishia kupotoea.
4) Tafuta suluisho la uwembamba wa mfumo hasa pale watakapo cheza na timu zinazotumia upana.
Deo Munishi
Ibrahim Shikanda
Erasto Nyoni
Said Mourad
Aggrey Morris
Abdulhalim Humud
Ibrahim Mwaipopo
Himid Mao
John Bocco
Abdi Kassim
Kipre Herman Tchetche
Juma Kaseja
Nassor Masoud
Amir Maftah
Paschal Ochieng
Shomary Kapombe
Ramadhan Chombo
Mrisho Ngassa
Mwinyi Kazimoto
Daniel Akuffo
Haruna Moshi
Emanuel Okwi
