top of page

Watani wa jadi wanakutana Jumatano hii katika uwanja wa taifa. Simba anaingia kwenye mechi hiyo ikiwa anaongoza ligi baada ya kushinda michezo zote minne. Yanga baada ya kusuasua wamafanikiwa kushinda mechi mbili mfululizo na hivyo kuwa nyuma ya Simba kwa alama tano. Hapa chini naelezea mambo machache yakutegemea kwenye mchezo  huo unao subiriwa kwa hamu na washabiki wengi nchini.

Mifumo
 

Simba itatumia mfumo wa 4-2-3-1 huku Yanga akitumia ule wa 4-4-2. Viungo watatu wa Simba amabo ni Kazimoto, Kiemba na Chombo watachuana na Chuji na Niyonzima. Chuji atacheza chini kidogo ya Niyonzima kama kiuongo mkabaji. Kutokana na kuwa na mchezaji mmoja zaidi kuliko Yanga kwenye safu hii basi tegemea Simba kutawala kwa kipindi kirefu cha mchezo. Mwenendo wa mchezo utakuwa kama ule wa Simba dhidi ya Ruvu Shooting.
 

Udhaifu katika upande wa Simba kwenye idara hii ya viungo upo kwa Kiemba ambaye anaonekana kupoteza pasi pale anapo kabiliwa na presha kubwa toka kwa wapinzani. Itakuwa vyema kama Yanga watatumia udhaifu huu na hivyo basi kawaweka katika nafasi ya kuanzisha mashambulizi ya ghafla pale ambapo watafanikiwa kumpora mpira. Ugumu ni kwamba kutokana na kwamba Simba ina viungo watatu huku Yanga ikiwa na wawili tuu si rahisi kuona Yanga wakifanya hilo. Jambo lengine kuhusiana na Simba ni kwamba Kazimoto uanza upande wa kulia lakini katika kipindi cha pili ubadilisha na kucheza upange wa kushoto.

Mpaka sasa Simba imekuwa ikitawala mechi zake zote na hii ni kutokana na mfumo wa 4-2-3-1 kuwa na viungo watatu katikati huko ule wa 4-4-2 ukiwa na wawili amabao timu nyingi bado wanautumia. Hivyo basi 4-4-2 unalemewa katika nafasi hii kwa kuwa na mtu mmoja pungufu yaani 3 v 2. Mfumo mzuri wa kukabiliana na 4-2-3-1 ni ule wa 4-3-3. 4-3-3 unahakikisha kwamba katika kila sehemu uwanjani idadi ya wachezaji ni sawa na hivyo basi matokeo ya mchezo yatategema sana uzuri wa mchezaji mmoja mmoja. Ili kuweza kuutumia huu ni muhimu kuwa kocha awe na imana na ufundi wa wachezaji. Ukizingatia kuwa katika mechi yao ya mwisho Yanga walionekana kumaliza mchezo wakiwa wamejipanga katika mfumo uliokuwa unafanana kidogo na 4-3-3 basi aitakuwa jambo la kushanga kuwaona wakitumia mfumo huo wakati wowote kwenye mchezo huo. Kama  Yanaga wataamua kutumia 40303 basi watatu wakati watakuwa Chuji, Damayo na Niyonyima.

Mabeki wa pembeni na mawinga
 

Kwanza kabisa ni dhahiri kuwa timu zote mbili zipo kamili katika nafasi za beki wa pembeni wa kulia, Twite wa Yanga na Cholo wa Simba. Kutokana na Maftah kupata kadi nyekundu na kutumikia adhabu yake itamlazimu kukosa mechi ya Jumatano. Jambo la kuzingatia ni jinsi namba hiyo itakavyo tafsiriwa na mchezaji atakaye cheza baada yake.
 

Ngasa upenda kuanzia upande wa kushoto na baada ya kupokea mpira kukimbilia ndani hivyo ni muhimu kwa atakaye chukuwa nafasi ya Maftah kupanda ili kujaza nafasi ambayo Ngasa uiacha kwa kukimbilia ndani. Hii itawapa Simba upana na pia itamlazimu Twite awe na mtu wakukabiliana nae.
 

Msuva upendelea kukaa pembeni na juu zaidi ukilinganisha na winga mwengine wa Yanga. Pili yeye ubadilisha upande. Kukaa kwake juu itamaanisha kwamba kama mabeki wa pembeni wa Simba watapanda wakati wa mashambulizi basi Twite au Joshua watajikuta wanakabiliana na maadui wawili. Itakuwa vyema Simba kuwa hamuru mabeki wake wapande maana itamlazimu Msuva kushuka chiji ili kumpa msaada beki wake na kwa kufanya hivyo watakuwa wamepunguza ukali wa mashambulizi ya Yanga hasa ukizingatia kuwa Msuva ndio aliyecheza vizuri mechi iliyopita. Pia inawezatokea kuwa kutokana na Msuva kucheza juu sana basi mabeki wa pembeni wa Simba kulazimika kutopanda sana ili kuboresha ulinzi wakati wanashambulia.
 

Kwa upande wa Yanga Joshua ni beki ambaye utetereka pale ambapo wapinzani wanapojaribu kumpora mpira hivyo basi washambuliaji wa pembeni wa Simba inabidi wajaribu kumpa wakati mgumu kadri iwezekanavyo. Hii itafanya mchezo wa Yanga utabirike kwa kuwa watakuwa wanaanza mashambulizi kwa goalkick au kwa kupitia upande wa Twite.

Mipira ya kona
 

Sunzu usimama karibu na mwamba wa kwanza pale ambapo Simba wana linda goli lao wakati wa mpira wa kona. Sababu kuu ni kuwalazimisha wapinzani kuning’iniza kona zao hivyo kumuwezesha Kaseja kuja kuzicheza. Hivyo njia rahisi ya kumkwepa Sunzu ni kucheza kona fupi. Kataika mchezo dhidi ya African Lyon Yanga walionekana kucheza zonal marking wakati wa kona na itaonekana kama wataendelea kutumia mbinu hiyo kwa michezo ijayo.

Mfumo wa 4-3-3 dhidi ya ule wa 4-2-3-1 uhakikisha kwamba kila kiungo pale katikati anakuwa na mpizani wake. Pia maeneo ya pembeni kila fullback anawinger wakukabiliana naye.

Juma Kaseja (c)                           
Nassoro Masoud                            .

?                              
Shomari Kapombe                    
Juma Nyoso                                 
Mwinyi Kazimoto                         
Amri Kiemba                                
Ramadhan Chombo                       
Edward Christopher                       
Felix Sunzu                                   
Mrisho Ngasa

Ally Mustapha
Mbuyu Twite
Oscar Joshua
Kelvin Yondani
Nadir Haroub

Idd 'Chuji'
Saimon Msuva
Frank Domayo
Didier Kavumbagu
Hamis Kiiza
Haruna Niyonzima

Mifumo na wachezaji wenye uwezekano mkubwa wakuanza mchezo wa kesho.

bottom of page