top of page

Juma Kaseja
Nassor Masoud
Amir Maftah
Paschal Ochieng
Shomary Kapombe
Mkude
Mrisho Ngassa

Mwinyi Kazimoto
Felix Sunzu
Amri Kiemba
Emanuel Okwi

Ally Mwadini
Ibrahim Shikanda
Sahm Nuhu
Said Mourad
Aggrey Morris

Abdulhalim Humud
Salum

Himid Mao
John Bocco
Jabir Aziz
Kipre Herman Tchetche

SIMBA 3 – AZAM 1: Azam washindwa kumudu mipira ya krosi

Simba: 4-2-3-1

Azam: 4-4-2 diamond

Simba inaendelea kuongoza ligi baada ya kufanikiwa kupata ushindi wa mabao matatu kwa moja dhidi ya Azam.  Ni mara ya pili kwa timu hizi kukutana, mara ya kwanza ikiwa katika mchezo wa ngao ya jamii. Simba ilikuwa na wiki nzima ya kujiandaa huku Azam ikiwa ni siku mbili tuu kutokana na kucheza katikati ya wiki.
 

Azam walitumia mfumo wao wa 4-4-2 diamond huku Simba 4-2-3-1 kama ilivyotegemewa. Kiemba na Mkude walicheza kama viugo wakabaji huku Kazimoto akicheza nyuma ya Sunzu. Kwa upande wa Azam, Humud ndio alikuwa kiungo mkabaji huku Salum akicheza nyuma ya Boko na Kipre Tchetche.

Dimba:

Azam walianzisha mashabulizi yao toka nyuma. Salum alikuwa akishika chini kuja kupokea mpira toka kwa Morad huku Humud akipanda. walijaribu kubadilishana hii nafasi ya kiungo mkabaji ila Humud ndiye alicheza pale kwamuda mwingi wa mchezo. Mfumo wanaotumia Azam unahitaji viungo wameze kuonana kwa pasi fupi fupi na za haraka ila hilo halikutokea sana na hivyo azam walipata wakati mgumu kupenya pale katikati. Mbinu ya kuu ilikuwa mpiria kwenye njia katikati ya mabeki wa kati na wa pembeni. Tatizo ni kwamba walikuwa wanaharakisha sana na pia simba walikuwa nawana bakiza mabeki watatu wakati wanashambulia ili kujilinda dhibi ya washambuliaji wawili wa Azam. Walifanikiwa katika kucheza mipira ya hewani na goli lao lilipatikana baada na Morad kupiga kichwa mbele ambacho Tchetche aliweza kupokea na kupenyeza pasi nyuma ya mabeki wa simba.

Simba waliweza kushambulia kwa kutumia upana wote wa uwanja. Okwi alikaa pembeni na hakiingia ndani sana kama ilivyo kawaida yake. Uwezo wa Simba kuhamisha mpira toka upande hadi upande kuliwahangaisha viungo wa Azam. Nafasi mbili zilitengenezwa kutokana na uwezo wa Simba kutumia upana wote wa uwanja. Ya kwanza ni pale Okwi alipo fanikiwa kupiga shuti lilogonga mwamba na ya pili ni hii iliyo sababisha goli la pili.

Pembeni:
 

Simba upenda kushambulia kupitia upande wa kulia. Hii ni kwa sabbabu ya kasi ya Ngassa na pia umahiri wa Masoud kujiunga kwenye mashambulizi na kupanda na mpira. Katika dakika saba za kipindi cha kwanza Simba walifanikiwa kuelekeza krosi mbili kuelekea lango la Azam.  Krosi ya kwanza Sunzu alikutana nayo ila mpira ukapita pembeni ya goli na ya pili muamuzi aliona kuwa Sunzu alimfanyia madhambi mlinda mlango wa Azam, Ally Mwadini. Kushambuliwa huku kulimlazimu Boko ashuke chini kuelekea upande huu ili kujaribu kumzuia Masoud asipande na mpira. Goli la kwanza lilipatikana kupita krosi ya Ngassa ambayo iwekwa nyavuzi na Sunzu.
 

Upande wa kushoto, ambako Okwi alianza hakukuwa na mashambulizi mengi. Shikanda alifanikiwa kumdhibiti Okwi na pia alikuwa akipanda wakati Azama wanashambulia na hivyo kuipa timu upana. Tatizo ni kwamba hakufanikiwa kumpita Maftah ila Azam walipata kona sio chini ya tatu upande huu. Kona zote hazikuwa na madhara yoyote kwenye lango la Simba. Goli la pili la simba nalo litokana na cross toka upande huu wa kushoto. Okwi alifanikiwa kuweka nyavuni krosi ya Kazimoto ambaye alipokea mpira wa kurushwa. Jambo la muhumi ni kwamba shambulizi hili lilianza upande wa kulia.
Kipindi cha pili Simba walianza mchezo kwa kasi na walifanikiwa tengeneza nafasi baada ya beki wa Azam kusita kuucheza mpira. Kazimoto alijikuta akikosa nafasi ya wazi, yeye na mlinda mlango. Goli la Okwi lilikuwa la uwezo binafsi na pia ilionekna kuwavunja moyo wachezaji wa Azam. Nafasi ya wazi ya Azam kipindi cha pili cha mchezo ilipakikana kupita krosi.

Bunjak vs Curkovic:

Kwa mara ya pili Curkovic amafanikiwa kumzidi maarifa mpinzani wake. Tukirejea mchezo wa ngao ya jamii, Curkovic aliwataka wachezaji wake washambulia kwa mapana katika kipindi cha pili ila hawakufanikiwa kutengeneza nasafi za wazi. Katika mcehzo wa leo, Simba walishambulia kwa mapana toka kipindi cha kwanza na pia kutumia mipira ya krosi kuelekea lango la wapinzani wao, jambo ambalo halikutokea katika mechi ya ngao ya jamii. Hii inaonyesha kwamba Curkovic aliweza kuona ni jinsi gani timu yake ingeweza kuongeza utengenezaji wa nafasi za wazi kupitia upana na mipira ya krosi.
 

Kwenye mchezo wa jana, ni mambo machache ambayo yanaridhisha kwa upande wa Azam.  Kweli, kuumia kwa Boko kulipunguza makali ya safu ya ushambuliaji ya Azam ila ukweli ni kwamba kwa mara nyingine wameshindwa kuficha udhaifu wa mfumo wanaotumia. Kufungwa ni moja ya matokea ya mchezo, ila kufungwa kwa njia hiyo hiyo, dhidi ya timu ile ile ni kitu cha kusikitisha na pia inaonyesha udhaifu katika benchi la ufundi.

bottom of page