top of page

Juma Kaseja (c)                           
Nassoro Masoud                            .

Paul Ngalema                        
Shomari Kapombe                    
Juma Nyoso                                 
Mwinyi Kazimoto                         
Amri Kiemba                                
Jonas Mkude                      
Edward Christopher                       
Felix Sunzu                                   
Mrisho Ngasa

Ally Mustapha
Mbuyu Twite
Stefano Mwasyika
Kelvin Yondani
Nadir Haroub

Idd 'Chuji'
Saimon Msuva
Nizar Khalfan
Said Bahanuzi
Hamis Kiiza
Haruna Niyonzima

Yanga walitumia mfumo wa 4-3-3 huku Chuji akicheza kama kiungo mkabaji. Khalfan alicheza kushoto kwake  na Niyonzima kulia ila juu zaidi ya Khalfan. Kazimoto alicheza nyuma ya Sunzu, Kiemba na Mkude walicheza kama viungo wakabaji.

Watani wa jadi wametoka sare ya moja moja . haikuwa mechi yenye kusisimua sana bali iliyojaa maarifa ya mchezo wa mpira. Brandts atakuwa ameridhishwa na sare ukizingatia kuwa  alijiunga na timu wiki moja iliyopita.

3 v 3 na ukabaji:
 

Kama ilivyotabiriwa na Trequartista, Yanga wacheza mfumo wa 4-3-3. Hii ilihakikisha kuwa pale katikati viungo watatu wa Simba watacheza dhidi ya viungo watatu wa Yanga. Simba ndio walitawala dimba . Yanga wali legalega kwenye hii idara kipindi cha kwanza huku tatizo kuu likiwa viungo wao kushindwa kutekeleza majukumu yao.
 

Viungo wa Simba, Kazimoto, Mkude na Kiemba walikaba vizuri, wakihakikisha kuwa kila kiungo wa Yanga alikuwa ana mtu pale anapo pokea mpira. Ukabaji wa Mkude ulikuwa mziri kiasi cha kumfanya Niyonzima kupotea kabisa pale katikati.
Katika idara hii, Yanga walikuwa na matatizo katika kushambulia na wakati wa ukabaji. Khalfan aliweza mkaba mpizani wake vizuri ila alikuwa anakaa na mpira sana na pia alikuwa anapiga pasi mbovu. Niyonzima aliweza mliki mpira vyema pale alipo upokea ila tatizo kubwa lilikuwa kushindwa kwake kumkaba Mkude. Alishindwa kuhakikisha kuwa anajiweka katikati ya goli lao na Mkude. Kutokana na kujipanga kwake vibaya, ilimaanisha kuwa wakati Simba wanashambulia, Chuji na Khalfan walikuwa wanashambuliwa na viungo wote watatu wa Simba.

 

Kuelekea mwisho wa kipindi cha kwanza, Domayo alingia akichukuwa nafasi ya Kiza. Khalfan alicheza kama mshambuliaji wa pembeni  huku Chuji, Domayo na Niyonzima wakicheza katikati. Wakati huo huo Niyonzima aliitwa kwenye benchi la ufundi na aliporudi uwanjani, alianza kuchukua nafasi katikati ya goli lao na Mkude. Kwa ufupi, Brandts alitatua matatizo yaliyokuwa yanawasibu.

Kipindi cha pili:

Kipindi cha pili Yanga walibadilisha mfumo  kutoka 4-3-3 kwenda 4-4-2. Niyonzima alianza kucheza winga wa kushoto ila kadri mchezo ulivyoendelea alihamia upande wa kulia. Maamuzi ya kubadilisha mfumo yalikuwa yakushanga kwa sababu kabla ya kipindi cha kwanza kuisha, Brandts alikuwa amefanikiwa kurekebisha makosa ya wachezaji wake. Ingekuwa vyema kama angeendelea  na mfumo wa 4-3-3 kwa angalau dakika kumi za mwanzo wa kipindi cha pili.
Mbadiliko hayo yalionekana kuwapa hamasa Yanga. Ilionekana kuwa Yanga walijaribu kumtumia sana Niyonzima . Kwa bahati mbaya, maamuzi yenye utata, rafu na kusimasima kwa mchezo ndio kuliharibu kipindi cha pili. Yanga walifanikiwa kutengeneza  nafasi mbili zote zikitokana na mipir mirefu kutoka kwa Twite na Ally Mustapha. Kona zisizo pungua nne za Yanga zilikuwa kona fupi. Waliajaribu kucheza kona fupi na Mwasyika kupiga shuti kuelekea golini.

Niyonzima:
 

Niyonzima ni mchezaji mwenye uwezo wa kumiliki mpira bila kuupoteza hovyo hovyo ila mchezo wa leo umeonyesha kuwa mapungufu yake yako kwenye ukabaji. Huu ni mchezo wa pili ambao ameshindwa kumdhibiti kiungo mkabaji wa timu pinzani. Katika mchezo dhidi ya Mtibwa, alipewa jukumu la kumzui Nditi asipate nafasi ya kucheza lakini alishindwa na hivyo kumfanya Nditi kutawala mchezo huo. Katika mchezo wa leo, kosa lake kubwa lilikuwa kushindwa kushuka chini na kuhakikisha kuwa anajiweka katikati ya goli lao na Mkude. Suala la yeye kubadilisha nafasi mara kwa mara ni tatizo pia. Mara acheze kama winga mara kiungo mshambuliaji. Pia ukiangalia maeneo anayokuwaakijiweka ni dhahiri kuwa anajiona kuwa yeye ni kiungo mchezeshaji. Yanga inabidi watafute ufumbuzi wa udhaifu wake wa ukabaji au hasiwe anausika kabisa katika ukabaji.

Hitimisho
 

Brandts alitambua umuhimu wa kubadilisha mfumo ili aweze kushindana katikaki ya uwanja. Kwa bahati mbaya, wachezaji wake walishindwa kutekeleza majukumu yao. Jambo lingine ni yeye mwenye kuto onyesha imani zaidi na maamuzi yake. Alifanikiwa kutatua matatizo ambao Yanga waliyapata kipindi cha kwanza ila akaamua kubadilisha na kucheza 4-4-2. Mkude, Kiemba na Kazimot walionyesha kuelewa nini Curkovic alihitaji toka kwao . ulikuwa mchezo wa maarifa sana, hasa katikati ya uwanja na ni bahati mbaya kuwa muamuzi aliharibu mchezo kwa maamuzi yake mabaya.

YANGA 1 - SIMBA 1 : Yanga wabadili mfumo mara mbili

bottom of page